Habari

Imewekwa: Dec, 21 2018

Kamat ya ujenzi ikiangalia na kukagua sehemu msingi ambako kumeshawekwa zege.

News Images

Kamati inayosimamia ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeridhika na kasi ya ujenzi wa msingi na uwekaji wa nguzo katika eneo ambako kunajengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Ihumwa. Timu hiyo ilipata maelezo kutoka kwa Injinia anayesimamia ujenzi huo Bw. Shadrack Ng'wizi ambaye alisema kazi inakwenda vizuri na siku ya ijumaa walitarajiwa kukamilisha ujenzi wa msingi.