Habari

Imewekwa: Mar, 22 2019

Mafunzo kazini ya Uandishi wa Sheria

News Images

Mwandishi Mkuu wa Sheria, Sarah Barahomoka amewataka Waandishi wa Sheria kuzingatia maadili , miiko na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amewataka pia kuzingatia mambo ya msingi yanayosimamia kazi zao. Akaitaja misingi hiyo kuwa ni Katiba ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Sheria mbalimbali pamoja na utunzaji wa siri.

Ameyasema hayo wakati wa mafunzo kazini kwa Waandishi wa Sheria watano ambao wamehamia hivi karibu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Divisheni ya Uandishi wa Sheria ( CPD)

Katika mafunzo hayo ambayo yalihusisha pia kupitia sheria mbalimbali, Mwandishi Mkuu wa Sheria, amewataka pia kuhakikisha kwamba wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia muda ( deadline). " Lakini msikimbilie kumaliza kazi kusudi muwahi muda wa kutoa kazi ile halafu mkaishia kutoa kazi ambayo ipo chini ya viwango, Hili nisingependa litokee au lifanyike. Zingatieni deadline lakini kazi lazima iwe ya viwango na ubora wa hali juu". Akasisitiza

Vile vile amewataka waandishi sheria hao kufanya kazi kwa umoja ( team work) kusaidiana na kushirikiana pasipo kubaguana