Habari

Imewekwa: Mar, 06 2019

MAFUNZO YA UELEWA WA VIASHIRIA HATARISHI YAHITIMISHWA

News Images

MAFUNZO YA UELEWAJUU YA VIASHIRIA HATARISHI YAHITIMISHWA

Mkurugenzi wa Mipangokatika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi Nkuvililwa Simkanga, amewataka watumishi waliopatiwa mafunzo ya Uelewa juu yaUsimamizi wa ViashiriaHatarishi, kujiandaa kuanzakuanda Mwongozo wa Ofisi wa Usimamizi waViashiria Hatarishi

Amayasema hayo siku yajumanne, wakati akihitimisha mafunzo ya siku mbili uelewa wa viashiria hatarishi yaliyotolewa kwamaafisabajeti wa kilaIdara na vitengo pamoja na maafisa watakaotambulika kama ‘Risk Champions’.

Mafunzo hayo ambayoyalitanguliwa namafunzo kwaWakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi naWakuu wa Vitengo yaliedeshwa na mtaalamuBw. Onesmo Mbekengakutoka Wizara ya Fedha na Mipango,Idara yaUkaguzi wa Ndani.

Bi. Simkangaamesisitiza kwamba kati ya sasa na mweziJune, hataka kamahakuna bajeti ya kazi hiyo, ni lazima kazi za awali za maandalizi ya Mwongozo huo zianze .

“ Hili la kuwa na Mwongozo wa Viashiria Hatarishi ni agizo la serikali, kwa hiyo lazima tuanzie mahali.Kati ya sasa na Junelazima tuwe tumefanya hatua za awaliza kuandaa huu Mwongozo. Mwanzo unaweza kuwa mgumu lakini tutaweza kama wote tuliopata mafunzo haya tukijituma”.

Na Kuongeza “ Hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali huwa anasisitiza kwamba, kuna vitu lazima vifanyike hata kama hakuna fedha kwa hiyo na sisi tufanya hivyo na ili kupeana hamasakila tunapokutana kuanzia sasa tuitane ‘risk champion’. akasisitizaMkurugenzi wa Mipango.

Wakati wa mafunzo hayo yakiwamo yavitendo, maafisa hao walijengewa uwezo wa namna ya kuainisha viashiria hatarishi, kutafuta njia za kukabiliana na viashiriahivyokabla havijatokeapamoja nanamna ya kuandaa mwongozo huo.