Habari

Imewekwa: Feb, 02 2019

OFISI YA MWANASHERIA MKUU IWE KILA MKOA-PM

News Images

OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI IWE KATIKA KILA MKOA-PM

Waziri Mkuu waKassim Majaliwa,ameishauri Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuhakikisha inakuwa naOfisi zake katikakila mkoa nchini ilikuwawezesha wananchi kupata ushauri wa kisheria kwa urahisi.

Ametoa wito huo leo( Jumamosi ) wakati alipotembelea Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo kufuatia maelezoaliyopewa alitaka kufahamu kama Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ipo katika kila Mkoa.

Waziri Mkuu alitembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea katikaViwanja vya Mwalimu Nyerere 'Square' Jijini Dodoma.' mara baada ya kuongoza maandamano yaliyowahusisha wadau wa Sheriawanaotekelezamajukumu yao kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya ufunguzi rasmi wa wiki yasheria ambayo kauli mbiu yake ni "Utoaji hukumu kwa wakati: Jukumu la Mahakama na Wadau".

Maandamano hayoya karibu kilomita tano yalikuwa nisehemu ya maadhimisho ya wiki ya sheria ambayokilele chake kitafanyikaFebruari 6, 2019 JijiniDar es Salaama na mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

" Kwa kuwa sasa mnaomuundo mpya namajukumu yenuyameongeza yakiwamo yauratibu na utoaji wa ushauri wa kisheria, jemna mnazo ofisi zenukatika mikoa yote". Akahoji WaziriMkuu nakuongeza " itakuwavema mkiwa na kuwa naOfisi kila mkoa iliwananchi wasisafiri umbarimrefukwenda kutafutaau kuomba ushauri wa kisheria".

Waziri Mkuuamesema anaamini kwamba baada ya mabadiliko ya kimuundo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalisasa inayo nafasi nzurizaidi ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi nakwa tija ni kwa sababu hiyo amesema kunahaja na umuhimu wakuhakikishahuduma za ushauri wa kisheria zinawafiki wananchi wa urahisi.

Awali akitoka maelezo kwa Waziri Mkuu, kuhusu majukumu yaOfisi ya Mwanasheria Mkuu hususani baadaya muundo mpya. Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Said Nzori amesema, baada yamabadiliko ya Muundo wa Ofisi hiyosasa ina Divisheni za kisheriatatu.

Akazitaja divisheni hizo kuwa ni Divisheni ya Mikataba ambayo jukumu lake nipamoja nakupitia mikataba ya kibiasharaya kitaifa na kimataifa pamoja na makubaliano ya kimataifaikiwa ni pamoja na kutoa ushauri kwaniaba ya serikali.

Kwa upande wa Divisheni yaUandishi waSheria, Bw. Nzori ameelezea majukumu yake kuwa nipamojana kuandaa miswada ya sheria kwa ajili ya kupitishwa na Bunge, na kuandaa hati zote za kisheria na maazimio kwa ajili ya kuidhinishwa na Bunge na kutafsri sheriakutoka lugha ya kiingereza kwenda kiswahili.

Akielezea zaidi kwa Waziri Mkuu kuhusu Divisheni za Kisheria katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa SerikaliBw. Nzori ameitaja Divisheni yatatu kuwa ni Divisheni ya Uratibuna Ushauri ambayo majukumu yake nikutoa ushaurikwa Wizara, Idara zinazojitegemea, mashirika yaumma, wakala wa Serikali za mitaa kuhusiana namchakato wa utungaji wa sheria na masuala mengine yanayohusu sheria.

Februari 13, 2918,Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Magufuli alitoa Amri ya KufanyaMabadiliko ya Muundo wa Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali.

Aya ya 3 ya Amri ya Muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyotangazwa katika Gazeti la Serikali Na.48 laFebruary 12,iliainisha madhumuni ya mabadiliko yaMuundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ni pamoja na pamoja nakujenga na kuimarisha uwezo na ufanisi katika uandishi wa Sheria na maazimio kwajili ya kujadiliwa naBunge, kujengana kuimarisha uwezo wa serikali katika kushughulikia mashauri yaliyofunguliwa mahakamani au kwenye mabaraza ya usuluhishi.

Madhumunimengine nikuongeza uwezo wa kutoa ushauri kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, mashirika ya umma, wakalana serikali za mitaa, wakalana serikaliza mitaa kuhusiana na mchakato wa utungaji wa sheria.