Habari

Imewekwa: Mar, 10 2019

OFISI YA MWANASHERIA MKUU KUTUMIA UZOEFU WA WASTAAFU WAKE

News Images

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa AdelardusKilangi amesema, Ofisi yake itaandaa utaratibu wa kuwatumia watumishi wake waliostaafu katika maeneo mbalimbali yakimamo ya kufundisha na ushauri.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki,( Ijumaa) wakati wa hafla ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi sabaambao wamestaafuna wanastaafuutumishi waumma kwa mujibu wa sheria. Hafla hiyona ambayo pia ilihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa ilifanyikakatika ukumbi wa Veta JijiniDodoma

Miongoni mwa watumishi hao wanaostaafu ni pamoja naMwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka , Mwanamke wa Kwanza kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria tanguTanzania ipate uhuru na amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 33.Miaka hiyo yote amefanya kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Watumishi wenzangu mnaostaafu.Mnastaafubado mkiwa naakili timamu na afya njema, mnastaafu utumishi wa Umma kwa Heshima kubwa hongereni sana. Uzoefu mnaoondoka nao hamkuupata kwa mwaka mmoja au mwili, ni uzoefu ambao umejijengea katika kipindi chote cha utumishi wetu” akasema Mwanasheria Mkuu .

Na kuongeza “ Ofisi yangututaandaa utaratibu wa kuangaliana namna ya kuutumia uzoefu wenu huu, iwe kwa kutoa ushauri au kwa kuja kufundisha. Na kwa hiyo msishangae mkiona hata katika ustaafu wenu tunawaomba mje mtusaidie katikakutuongezea nguvu katika maeneo fulanifulani mkiwa kama washauri au wakufunzi.Na ninaomba sana tutakapowaomba na kuwahitaji mtukubalie” akasisitiza nakushangiliwa na watumishi.

Profesa Kilangi amewataka wastaafu haokwenda na kuutumia uzoefu wao waliojijengea katika utumishi wa umma kwa maendeleo na manufaa yaowenyewe na familia zaolakini piakwa manufaa na maslani pamana yaSerikali naNchi kwa Ujumla.

Kuhusu watumishi wate wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Kilangi amewashukuruna kuwapongeza kwa namna ambavyo wameupokea na kuanza kuutekeleza Muundo Mpya wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatiamabadiliko yaliyofanya na Mhe Rais John Magufuli mwakajana.

“Niwashukuruni sana kwa namnamnavyotekeleza majukumu yenu, wengi wetu tumeyapokea vema mabadiliko yaMuundo wa Ofisi aliyoyafanya Mhe Rais mwaka jana nammeelewa lengona nia yake ambayo ni kuboresha huduma zinazotolewa na Ofis yaMwanasheria Mkuuwa Serikali na nipende kusema mbele yenu kwamba sasa ukizungumza na wadau wetu wengi huko nje wanafurahi sana, wanaridhikasana na huduma zinazotolewa naOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali” akasema .

Pamoja na pongezi hizo, amewataka watumishi wote wa Ofisiyake ni vema wakafahamuulimwengu wa sasa unahitani watu auwatumishi wasomina wenye uwezo wa juu wa kuelewa mambo na kutatua matatizo na katika muktadha huo ametoa wito wa watumishi wotekila mmoja kwa mujibu wa kada yake kujiendeleza ili Ofisi ya MwanasheriaMkuuwa Serikali ikawe kioo na kielelezobora katikaTaifa letu.

“Natoa witomjiendeleze kwakulingana nakada zanu mwenyecertificate basi apatediploma, mwenye diploma apate degree ya kwanza na mwenye degree ya kwanza apate ya pili na na mwenye ya pili alenge kupata udaktari na hatimaye uprofesa hakuta kuwa na shinda kama ofisi hii itajaamadokta” akasisitizakwa mkazo.

Pia amewataka watumishi wote kujiandaakifikra kwa mapokeoya matumizi ya tehama katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku pamoja na kutumia vema muda wa kazina kutumia vema raslimali na vitendea kazi vilivyovopoili kutekeleza vemana kwa tija kauli mbiu ya ‘hapa Kazi tu’

Aidha amesema anaridhiswa na kufurahishwa na idadikubwa ya watumishiwanawake ambao wameshika nafasinaWakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Vitengo utaratibu ambao amesema ameukutahataka kabla yake.

Akitoa salamu za Shukrani kwa niaba ya wastaafu wenzie Mwandishi Mkuu wa SheriaBibi Saraha Barahamoka amemshukuruMwanasheria Mkuu wa Serikalikwa kuwaandalia hafla ya kuwapongeza na kuwaaga ikiwa ni pamoja na kuwapatia vyeti vya utumishi.

Akasema yeye binafsi na wenzake wamefurahishwa sana na namna Ofisi ilivyotambua na kuthamini mchango wa utumishi wao katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Serikalina Nchi kwa Ujumla.

Aidha akasema,katika kipindi chote cha utumishi wao katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamepata ushirikiano mzuri kutoka kwaviongozi wa juu na watumishi wenzaona kwamba wanaomba ushirikiano na moyo huo wa kusaidianaunaendelezwabaina ya viongozi wa wajuu na watumishi wote.

Watumishi wengine waliostaafu ni Bibi Ester James Manyesha ambayeni MkurugenziMsaidizi Uandishi wa Sheria na amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 35, Bibi Grace Mlondezi Mfinaga, Mwandishi waSheria Mkuu Daraja lakwanza na amekuwa katika utumishi wa umma kwa Miaka 36 na Bw. Hussein ShabaniKaweto Msaidizi Kumbukumbu Daraja la kwanzaambaye amedumu katika utumishi wa Umma kwa Miaka 37.

Wengine ni Bibi. Benadetha Cosman Karadisyambaye ni Msaidizi wa Mtendaji MkuuDaraja la Pili na amedumu katika utumishi wa Umma kwa miaka 36, Bw. Cosmasi Bayi Machupaambaye ni Dereva daraja laKwanza yeye amedumu katika utumishi wa Umma wamiaka 16 na Bibi Mary Mahigu Maganga ambaye niMsaidizi wa Ofisi Mkuu yeye amedumu katika utumishi wa Ummakwa miaka 30