Habari

Imewekwa: Mar, 08 2019

Wanawake Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waungana na wenzao kusherehekea siku ya Wanawake Duniani

News Images

WANAWAKE OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI WAUNGANA NA WANAWAKE WENZAO KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Wanawake katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo Ijumaa wameungana na wanawake wenzao Duniani katika kuiadhimisha sikuya Wanawake Duniani

Wanawake hao wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mipango Bi. Nkuvililwa Simkanga, na wakiwa wamevalia sale zao za kupendeza na nyuso zilizojaa bashasha . Walishirikia maandamano yaliyoanzia Uwanja na Jamhuri na kupokelewa katika Viwanja vya Mashujaa na Mhe. Antony Mavunde, NaibuWaziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayehusika namauala ya Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu

Machi 8 ya kila mwakaimetengwa kama siku ya Wanawake Duniani, ni siku ambayo wanawakehukutana na kubadilishana mawazokuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mstakabali waoikiwa pia nakuzijadili changamoto zao na namna yakuzikabili.

Kauli mbiu yamaadhimisho yamwaka huu ni “ Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa MaendeleoEndelevu”